Mlevi Mwala alishindwa kufikia Breki kabla ya Ajali- Polisi

Image result for inspector mwala

Mcheshi Davis Mwabili anayejulikana kama Inspekta Mwala ameachiliwa kwa dhamana ya Shilingi 40,000 akisubiri kesi kusikizwa. Anashtakiwa kwa kosa la kumuua mtu kupitia ajali ya barabarani iliyofanyika Kilifi Jumatatu usiku.

“Mshtakiwa sharti afike kortini Ijumaa wiki ijayo kujibu shtaka la kuua kwa kuendesha gari kiholela.” Mkuu wa Polisi wa Rabai David Maina alisema.

Polisi wanadai kuwa alimgonga na kumuua mtu aliyekuwa akitembea kwa miguu. Mwala ambaye anaigiza kama Mkuu wa polisi katika kipindi cha ucheshi- Inspekta Mwala- alijikuta katika upande mbaya wa sheria.

Polisi wanadai mcheshi huyo alikuwa amelewa wakati wa ajali iliyotokea mwendo wa 11.00 jioni alipokuwa akiendesha gari kwenda Kaloleni kutoka Mazera.
Maina alithibitisha kukamatwa kwa Mwabili Jumanne.

Image result for inspector mwala

“Tulimkamata mshukiwa huyo kutoka eneo la tukio hadi kituo cha Polisi Rabai baada ya kumuokoa kutoka kwa umati uliojawa na hamaki na tunamshikilia kwa uchunguzi,” alisema OCPD.

Polisi pia wanadai kuwa ajali hiyo ilitokea wakati mhusika alipojaribu kulipita gari lililokuwa likuja upande wake na hapo ndipo alipopoteza mkondo, na akamgonga mtu aliyekuwa makitembea kwa miguu. Muigizaji alikuwa peke yake kwenye gari husika na inasemekana hakuweza kufikia breki.

Polisi walisema gari la mshukiwa lilimvuta marehemu kwa umbali wa mita 100, na kumjeruhi vibaya kwa kumgonga fuvu lake, mikono na miguu kabla ya kusimama.

Maina aliliambia gazeti la The Standard kwamba walipopata habari ya ajali hiyo, polisi walielekea la tukio na kumuokoa mshukiwa ambaye alikuwa amezungukwa na wakaazi waliojawa mori .cPolisi walipiga risasi hewani kuwatawanya waendeshaji wa pikipiki waliojawa na hamaki.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika hifadhi la maiti la Pwani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *