Nafasi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Bajeti zi Wazi- Uhuru

President Uhuru Kenyatta.

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa nafasi katika ofisi za Mukaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Bajetizi(CoB) zi wazi.

Stephen Masha ameteuliwa kuwa Msimamizi wa Bajeti kwa kaimu kwa muda wa siku 90, na kuanzia Agosti 27.Masha hapo awali alikuwa naibu Mdhibiti wa Bajeti. Anashikilia shahada ya pili ya Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Leicester nchini Uingereza na ni mhasibu wa umma aliyehakikiwa.

Nafasi za Mhariri Mkuu na CoB zilitangazwa kuwa wazi baada ya muda wa Edward Ouko na Agnes Odhiambo kumalizika baada ya kipindi cha miaka nane .

Ili kuhitimu katika kazi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na CoB, lazima mtu awe na tajiriba ya miaka 10 katika usimamizi wa fedha za umma au ukaguzi. Wanapaswa kuwa na digrii katika kifedha, uhasibu au uchumi.

Wale wanaoangazia kitiĀ  hiki wanapaswa kuwa wametimiza majukumu yao yote ya ushuru.

Maombi ya kazi yanaalikwa hadi Septemba 9 saa 5 jioni na yanapaswa kuelekezwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Huduma ya Umma (Public Service Commission).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *