Masaibu ya Mchungaji Ng’anga – Waaumini watishia Kumfungulia Mashtaka

Image result for pastor nganga

Mchungaji James Nganga wa  Neno Evangelism Minitries kwa mara nyingine tena amejipata katika mtego thabiti wa sheria.

Waaumini wa kiume hawakufurahishwa na tishio lake la wakata sehemu zao za kiume iwapo wangemdharau. Tamko hilo liliambwa alipokuwa akiwahubiri mbele madhabahu kanisani humo.

Waumini hao kupitia  mawakili wa Otieno & Amisi Advocates, wameapa kuchukua hatua kisheria iwapo Mchugaji hangeomba radhi. Nganga anashutumiwa kuwa mwingi wa kiburi na kutumia lugha isiyo na tasfida mbele ya Madhabahu.

“Unashutumiwa kwamba tarehe tofauti ulitumia maneno ya kutishia na matusi kwa kusudi la kuvunja amani … na haswa kwa kutumia ishara kuwadharau kwa kulinganisha uume wao na kidole cha pili ,” ilisoma sehemu ya barua ya wakili.

Waumini hao sasa wanataka, Nganga aombe msamaha kati ya siku mbili au mashtaka ya Kuwafedheha kufunguliwa.
“Vitendo vyako  vimewafedheha na kuwachafulia taswira waumini wa kiume machoni pa jamii na kuwafanya kama waoga na wasio na akili timamu,” wanasheria waliaandika.

Shutuma hii inakuja siku moja baada ya Mchungaji Ng’anga kuomba msamaha kwa mwandishi wa Citizen TV Linus Kakai kwa tishio la kifo aliyotoa dhidi ya maisha yake Machi mwaka huu.

Alitoa msamaha rasmi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Patricia Gichohi katika Korti za Kiambu. Mnamo Mei Mchungaji Nganga, aligonga vichwa vya habari baada ya video yake akiwakemea maaskofu  ya Kanisa lake dhidi ya kumdharau yeye na mkewe kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Kutokana na video hiyo, Robert Wafula wa askofu mkuu katika kanisa hilo alijiuzulu. Alisema alikasirika kwamba mwanaume ambaye amemfahamu kwa zaidi ya miaka 20 angechukua kipaza sauti na kuwashambulia hadharani.

“Kama angekuwa na maswala yetu, angepiga simu kwa mkutano. Lakini kutangaza hadharani kwamba atatutoa inamaanisha hataki kufanya kazi na sisi. Ningependa kuondoka kuliko kungojea afanye kile alichotishia, “anasema Wafula.

Mchungaji Nganga bado hajatoa tamko lake kuhusu  suala hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *