Bobi Wine anapaswa kujiunga nasi kama hawezi kutushinda- Museveni

Image result for museveni and bobi wine

Rais Yoweri Museveni amesema kuwa mbunge wa Kyandondo mashariki Bobi Wine hapaswi kutumia fujo ili kumtoa mamlakani bali kuwashawishi Waganda.

Rais siku ya Jumatatu alikuwa akijibu maoni ya waganda kwenye mtandao wa kijamii akiwa njiani kuelekea nchi ya Japan.

Mmoja wa wafuasi wa Museveni alitoa maoni yake akisema kuwa kama Bobi Wine anataka uongozi aende msituni akapigane.

Walakini, Museveni alijibu kuwa Bobi Wine aendelee utoa ajenda zake kwa wananchi ili kuwashawishi na kama atashindwa basi ajiunge na chama tawala cha NRM.

Image result for museveni and bobi wine

Hiyo ‘kwenda msituni sio lazima’ aliongezea Museveni.

“Siasa ni kuuza sera. Kama hawana sera basi watafute kwani sisi tumeweka sera zetu mbele ya wananchi. Kama watashindwa basi wako huru kujiunga nasi.”

Leo mapema, Bobi Wine alitangaza kuwa anamalizia sera zake za ‘Uganda Mpya’ kabla ya uchaguzi mkuu wa 2021.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *