Jubilee kupendekeza Mgombea katika Uchaguzi mdogo wa Kibra

Jubilee secretary general Raphael Tuju addressing the media on the Wajir West By election on April 10, 2019.

Chama cha Jubilee kitatoa mgombea katika uchaguzi mdogo ujao wa Kibra, katibu mkuu wa chama hicho Raphael Tuju amethibitisha.

Kupitia taarifa aliyotoa Jumatatu Tuju alisema chama hicho, baada ya kushauriana ndani ya uongozi wa chama , wameamua kutoa mgombea.

“Tunapenda kuwaambia wanachama kwamba chama cha Jubilee kitakua kinampendekeza mgombea katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kibra mnamo Novemba 7, 2019,” Tuju alisema.

Tuju alisema kuwa uchambuzi wao na mashauriano yanathibitisha kuwa Chama cha Jubilee kina ushindani wa kutosha katika mashindano ya kisiasa yanayokuja.

“Ni muhimu kukumbuka kuwa eneo jirani la Lang’ata  lilimchagua mgombeaji wa Jubilee kinyume na uchambuzi  wa kisiasa. Kwa hivyo tunatoa taarifa kwa wanachama wetu ambao wana nia ya kugombea kiti hicho kwa tiketi ya chama cha Jubilee, kujisajili kwenye bodi ya uchaguzi wa kitaifa.”

Tuju alisema kuwa watazingatia maagizo kwa mujibu wa maagizo ya NEB ya chama.

Tangu Machi mwaka jana, baada ya maafikiano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga, vyama vyote  viwiili zimeheshimiana na havijapendekeza wagombea dhidi ya mpinzani katika uchaguzi mdogo wa Wajir Magharibi, Embakasi Kusini na Ugenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *