Ujumbe wa mke wa kwanza wa De Mathew wafanya waombolezaji kuambulia vicheko

Wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu John Ng’ang’a almaarufu De ‘Mathew, Jumamosi, mkewe wa kwanza, Sarafina Wairimu John, aliuliza wanahabari wasiingilie kati yake na mke wa pili, Carolyne Waithera.

Alisisitiza kwamba wakati mwanamuziki huyo alikuwa hai, wawili hao hawajawahi kukuwa na mgogoro wowote.

“Mtu asije akatuingilia kati yetu. Carolyne ameniheshimu, mimi ni mama Shiku, na yeye ni mama Mathew na hatutaki mtu yeyote aje kati yetu, “alisema.

Sarafina alisimulia tukio moja ambapo De Mathew alisahau shati lake nyumbani kwa Caroline, na kumfanya aulize ikiwa shati hilo lilikuwa kwake.

De' Matthew's first wife, Sarafina Wairimu John, second wife Carolyne Waithera, President Uhuru Kenyatta and Deputy President William Ruto on 24/8/19

“Ikiwa kabisa namuuliza maswali na yeye anajibu kwa heshima, basi ni nani anayeweza kuja kati yetu?” aliuliza.

Mke wa kwanza wa De Mathew aliendelea na kusema kuwa watoto wake na wale wa Caroline wanaishi pamoja kwa maelewano, na kuongeza kuwa hakuna kitakachobadilika hata baada ya kifo chake.

“Ninampenda na ninamuheshimu Caroline. Alinifuata na anajua nilikua nimemtengenezea mzee. Nitasimama na kuchukua majukumu ya John, “alimwambia Caroline, akiwaacha waombolezaji wakipasuka na vicheko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *