Waiguru asherehekea kushtakiwa Upya kwa Kabura

Kirinyaga Governor Anne Waiguru.

Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru amefurahia hatua ya kumshtaki mfanyabiashara Josephine Kabura upya kutokana na Sakata ya NYS. Gavana huyo katika ukurasa wake wa twitter, jumanne, alisema kwamba mashtaka dhidi ya Kabura yamehairishwa kwa muda mrefu lakini mwishowe haki itatawala.

Aliendelea kunukuu sehemu ya Wimbo wa Kitaifa: “Haki iwe ngao yetu na mlinzi.”

Waiguru alisema, “Bado ninangojea ashtakiwe kwa kuapa kiapo cha uwongo mbele ya mahakama na mashtaka dhidi ya waandani wake … Kuna Mungu mbinguni, haki inapaswa kutawala.”

Kabura, ambaye amehusishwa na wizi wa pesa za Shillingi milioni 791 za NYS na kisha mnamo Jumanne alishtakiwa tena  kwa sababu ya  utapeli wa pesa.

Inadaiwa kuwa Kabura, John Kago Ndungu na Patrick Ogolla kati ya Desemba 2014 na Mei 30, 2015, walihusika katika njama ya uhamishaji wa Sh90 milioni kwa akaunti katika Benki ya K-Rep inayomilikiwa na Patrick Ogolla Onyango and Company advocates.

Businesswoman Josephine Kabura with other suspects linked to the theft of NYS funds at a Milimani Court on Tuesday, August 20, 2019.

Katika kesi hiyo, Kabura anashtakiwa pamoja na mfanyabiashara Ben Gethi, John Kago, Samuel Wachenje, wakili wa Patrick Ogolla, Anthony Gethii, Benson Gachoka, John Hope Vandamme, Martin Wanjohi, Charity Wangu, na Jedidah Gethi.

Watuhumiwa walikana makosa 16 yanayohusiana na shughuli ambazo kiongozi wa mashtaka anasema yanahusisha fedha zilizoibiwa.

Upande wa mashtaka ulimweleza hakimu Martha Mutuku kuwa Kabura na washtakiwa wenzake walihamisha pesa hizo huku wakifahamu fika kuwa ni fedha za utapeli katika NYS.

Kiongozi wa mashtaka alieleza mahakama kuwa washatakiwa walijilimbikizia mali ikiwa ni pamoja na magari, viwanja, na nyumba kwa kutumia pesa za NYS kupitia kampeni zilizoficha uongozi wake.

Mashtaka dhidi yao inasema kuwa kati ya Desemba 1, 2014, na Aprili 30, 2015, jijini Nairobi, waliungana kwa pamoja katika mpango wa ununuzi wa magari kwa gharama ya Sh23 milioni huku wakijua kuwa pesa hizo zilikuwa ni za uhalifu.

Kabura na Kago walikana kwamba walinunua gari inayogharimu Sh6.3 milioni kutokana pesa za sakata ya NYS

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *