Museveni na Kagame waafikiana juu ya mzozo wa mipaka

Image result for museveni and kagame

Rais Museveni na mwenzake Paul Kagame Jumatano wiki hii wanatarajiwa kuafikiana nchini Angola kwa malengo ya kusitisha mgogoro kati ya nchi zote mbili na kupelekea kufunguliwa kwa mipaka ya Rwanda-Uganda.

Chombo cha habari cha China, Xinhua, iliripoti kuwa rais wa Angelo Joao Luarenco atahudhuria mkutano itakayofanyika Luanda kuashiria maafikiano kati ya Rwanda na Uganda.

“Rais wa Uganda na Rwanda watakutana kwa Jiji kuu la Angola Agosti 21 ili kufikia maelewano wa mipaka wa nchi zote mbili,” Xinhua inaripoti.

Image result for museveni and kagame

“Rwanda na Uganda ilikutana kuongea baada ya Angola na Demokrasia ya Kongo kusaidia kwa majadiliano ya jirani yao,” Xinhua pia iliongezea.

Mkutano huo wa wiki chache zilizopita kati ya Museveni na Kagame pia ilikusudiwa kuimarisha usalama kati ya nchi nne, Kongo, Uganda, Rwanda na Angola.

Kutoka Februari mwaka huu, Rwanda imefunga mipaka yake na kuzuia wafanyibiashara wa Uganda wanaobeba mizigo kwenye nchi hiyo.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *