Serikali kutumia Mamilioni Kikarabati Makavazi ya Jaramogi Oginga Odinga

Makavazi ya Jaramogi Oginga Odinga huko Bondo yatapata fahari kubwa baada ya Kutengewa pesa za kukarabati. Gharama ya shughuli hiyo inakadiriwa kufika milioni 8. Hii inakuja baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuamuru ukarabati alipotembea nyumbani kwa Jaramogi mnamo Disemba 14, 2018.

Shirika la Makavazi ya Kitaifa  (NMK) pia limetenga zaidi ya shilingi Bilioni 2 ambazo zitaelekezwa katika kukarabati zaidi ya vituo 100 kote nchini.

Kutokana na ripoti zilizotufikia, Shughuli hizo zinatarajiwa kuanza ifikapo mwezi wa agosti.

Mkurugenzi Mkuu wa NMK Mzalendo Kibunjia alikuwa katika mkoa huo akikagua matayarisho ya ukarabati wa Jumba la Makumbusho la Jaramogi, kule Kango ka Jaramogi, nyumbani kwa Makamu wa Rais wa kwanza wa Kenya.

Kibunjia alithibitisha kwamba ukarabati uliopangiwa jumba hilo la makumbusho uko kwenye mkondo. Katika hafla hiyo ,alitangaza kuwa kazi za ukarabati zilikuwa zimeanza, na kuongeza kuwa sehemu hizo zitakazorekebishwa zina umuhimu wa kihistoria kwa nchi.

Baadhi ya vituo vinavyosubiri ukarabati vimekuwepo kwa miongo mingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *