Serikali kutumia mamilioni Bondo kwa heshima ya baba mzazi wa Raila

Serikali imedhamiria kutumia mamilioni ya shilingi kwenye muundo wa kipekee kwa heshima ya baba mzazi wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Jumba ya makumbusho ya Jaramogi Oginga Odinga huko Bondo itakarabatiwa kwa gharama inayokadiriwa ya shilingi milioni 8.

Hii inakuja baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuamuru ujenzi huo ubadilishwe wakati alipotembelea nyumbani kwa Jaramogi, hapo nyuma Disemba 14, 2018.

Jumba la Makumbusho ya Kitaifa ya Kenya (NMK) pia lilianzisha mpango wa ukarabati kwa shilingi bilioni mbili ambao utaona vituo 100 vya urithi vikirekebushwa.

Image result for jaramogi oginga odinga museum

Mratibu wa Mkoa wa NMK huko Nyanza, Daniel Mitei, alithibitisha kwamba zoezi hilo linastahili kuanza Agosti, Ripoti ya Capital Fm ilieleza.

Mitei alizungumza Jumatano, alipompokea Mkurugenzi Mkuu wa NMK, Mzalendo Kibunjia, kule Kisumu.

Kibunjia alikuwa katika mkoa huo kukagua matayarisho ya ukarabati wa Jumba la Makumbusho la Jaramogi, huko Kango ka Jaramogi, nyumbani kwa Makamu wa Rais wa kwanza wa Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *