Mama mzazi wa Wendy Waeni Ni mlevi, Joe Mwangi Adai

Image result for joe mwangi and wendy waeni

Maji yamezidi unga na imebaki sheria kuchukua mkondo wake katika hadithi ya Wendy Waeni ambayo Joe Mwangi ameikataa.

Mambo yamechukua mkondo mwingine baada ya Joe Mwangi kufanya mahojiano na mcheshi Chipukeezy kwenye televisheni ya Ebru.

Wendy Waeni alishtua wengi alipokiri kuwa meneja wake wa zamani alimwacha mlala hoi ata baada ya kupata fursa ya kuzuru nchi za ng’ambo ikiwemo China na Ujerumani.

Image result for joe mwangi and wendy waeni

Nilimpa mama wa Wendy shilingi elfu mia moja (100000) kumlipia ada yake ya shule lakini yeye ni mlevi

Joe Mwangi alithibitisha kwamba Wendy hajawahi kufanya sarakasi kwa miaka miwili na kama msanii, mtu anaweza kulipwa tu wakati anaalikwa kutumbuiza.

Mara ya mwisho Wendy alitumbuiza ni miaka miwili iliyopita, amekuwa shule na hakuna jinsi atakavyolipwa  kama hatumbuizi.

Wakenya sasa wamebaki katika hali ya sintofahamu wasijue ni nani wa kumwamini na nani wa kumkemea.

Haya ni baadhi ya maoni yao;

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *