Ruto akosa kuhudhuria mikutano 8 ya baraza la mawaziri

Image result for cabinet meeting in kenya

Tofauti kwenye baraza la mawaziri imeendelea kuonekana ikileta athari kwa sekta mbalimbali za kiserikali.

Kupitia ripoti ya televisheni ya Citizen, kupandishwa cheo kwa waziri wa mambo za ndani, Fred Matiang’i kwenye baraza la mawaziri haijapokelewa vizuri.

Kwenye kipindi cha usiku, Linus Kaikai aliuliza kama rais alifanya vizuri kwa kumweka matiang’i kuongoza mikutano ya baraza la mawaziri na kumtarajia naibu rais William Ruto kuhudhuria.

Waziri wa zamani na pia balozi wa Kenya nchini marekani, Burudi Nabwera aliongea na televisheni ya Citizen akisema kuwa “mikutano ya baraza la mawaziri linakutana kila wiki ii kuongelea mambo yanayosibu nchi.”

Nabwera ambaye alifanya kazi kwenye serikali mbili za Kenyatta na rais mstaafu Daniel Arap Moi alisema kuwa mikutano haikuwahi feli na labda tu wakiwa wametoka nje ya nchi.

Image result for burudi nabwera

Msemaji wa ikulu Kanze Dena alisema siku ya Jumanne kuwa hakukuwa na suala la kuongelea yenye dharura kwa mkutano wa Alhamisi.

Kama kawaida, mikutano ya baraza la mawaziri inafaa kusimamiwa na naibu rais kama rais hayuko lakini cheo kilimwangukia waziri Fred Matiang’i.

Kwenye ripoti ya Alhamisi, NTV ilisema kuwa baraza halijakutana kwa mara nane mfululizo na mawaziri wamekataa kuwa hawana tafouti kati yao.

“Usikilize mtu yeyote ambaye ana muda wa kupoteza. Tunafurahia uhusiano mzuri na unaweza kuona kwamba sisi ni ndugu na dada kweli, “Matiang’i alizungumza hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *