Hakuna stesheni ilitaka kufanya kazi nami- Wanjiku aeleza maisha yake baada ya kutolewa Citizen

Related image

Msanii na mcheshi Teacher Wanjiku amefichua kilichompelekea kupotea kwake mwaka wa 2014 baada ya kuteka nafasi ya juu kwenye ulingo wa ucheshi.

2014 ndio mwaka ambayo mti wake ulianguka. Hii ni baada ya kupata kazi kwa televisheni ya Citizen kwenye kipindi chake cha darasani ambapo alifanya ucheshi wake.

Lakini hii haikudumu, kwani baada ya wiki moja, kipindi chake kilitolewa kwa sababu haikufikia matarajio fulani kwenye sekta hiyo.

“Nilifikiria nilikuwa nimekipata lakini nilifeli kabisa,” Wanjiku alikubali.

Kati ya vitu ambavyo Wanjiku anaamini vilichangia kufeli kwa kipindi chake ni uvumi kwamba alitoka ‘vibaya’ kwenye Churchill Show.

Image result for teacher wanjiku

Hii ilimharibia biashara zake na pia makampuni na vyombo vya habari havikutaka kujihusisha na yeye.

“Hakuna mtu alitaka kunisikiliza. Kulikuwa na siasa nyingi na uvumi kuhusu ni nini kilinipelekea nikaondoka Churchill. Hakuna kituo cha waandishi wa habari kilichotaka kufanya kazi nami. Nilipoteza marafiki. Nilikuwa na uchungu na hasira, “alikiri kwa True Love Magazine.

Baada ya hii, maisha yake ilibadilika sana na akaliuza gari lake la dhamana na akarudi kwenye msigi wake wa kutathmini ni vipi atarudi kwenye ngazi ya juu.

Hata hivyo, Wanjiku hakutamauka kwenye kazi yake na akatumia mtandao wake, haswa Facebook kwa ucheshi wake kwenye video za ‘Aunty wa Harrier’ kilichomsaidia kukuza wafuasi wake.

Kwa sasa, Teacher Wanjiku amerudi kileleni na hivi majuzi tu alishinda tuzo pale marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *