Wakati mgumu kwa makampuni ya michezo ya kamari huku kuhamishwa ni athari kwao

Image result for betting firms in kenya

Maji yanazidi unga kwa makampuni ya michezo ya bahati nasibu na kamari huku serikali ikitafuta njia ya kufuta leseni za baadhi yao.

Kwa mujibu wa People Daily, wizara ya mambo ya ndani inapanga kuwahamisha wageni wote wanaofanya kazi na kampuni za michezo ya kamari.

Gazeti hilo liliendelea kusema kuwa baadhi ya wafanyikazi hao waliigia nchini kutumia visa za utalii.

Hii inatokea siku mbili baada ya rais Uhuru Kenyatta kusema kuwa hatong’atuka kwa mabadiliko kwa sekta hiyo.

Alisisitiza kuwa hatabadilisha maamuzi ya serikali ya kutoa mfumo wa malipo na uumbe kwa kampuni 27 mpaka wapewe leseni mpya kulingana na sheria.

Juma lililopita, Waziri fred Matiangi aliwashauri wateja kutoa pea zao katika masaa 48 kabla malipo ya Mpesa kutolewa hadi makampuni yafuate vipengee vya sheria.

Kwenye kumbukumbu, mwezi wa Mei, serikali iliwahamisha wageni 17 ambao walipatikana wakifanya biashara ya kamari kinyume na sheria.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *