Msanii wa injili akiri kuwa na uraibu wa ngono

Image result for nicah the queen

Msanii wa kike wa injili, Nicah The Queen amefichua kwa mashabiki wake kuwa maisha yake sio ya kikamilifu na sahihi.

Nicah amelezea kuwa hata ingawa ana picha nzuri kwa mashabiki, amepitia changamoto nyingi kwenye maisha yake ya kukua.

Aliwaeleza mashabiki wake kwenye mtandao kuwa alikuwa karibu kukuwa kahaba kwa namna ya ngono.

Image result for nicah the queen

Nicah alipata malezi kwa baba yake baada ya mama yao kuwakimbia akiwaacha nyuma na ndugu zake wadogo na maisha haijakuwa ya raha mustarehe.

Maji yalizidi unga alipofika miaka kumi na mitano baada ya kupata ujauzito wa kijana wa miaka 26 na alimtoroka alipojua kuwa alitarajia mtoto.

Image result for nicah the queen

Kama tu mtu yeyote asiye mkamilifu kama mkristo, alifichua siri zake na jinsi anang’ang’ana na uraibu wa ngono na akawahimiza wanaopitia changamoto pia wazungumze.

“Siogopi kuzungumzia masaibu yangu, mwito wangu sio takatifu, nitasema na kurudia kwamba nipo hapa leo kwa sababu ya vitu ambavyo nilivipitia. Niko hapo kupea nguvu yule dada anang’ang’ana na uraibu wa ngono, ukahaba, na masahibu mengine, nitaendelea kueneza ujumbe hu mashuleni, Mungu nipe nguvu,” aliongezea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *