Zari atangaza tarehe ya harusi nchini Kenya

Zari Hassan announces wedding date upon landing in Mombasa

Mwanamtindo na mfanyibiashara mashuhuri wa Uganda, Zari Hassan, hatimaye ametangaza tarehe yake ya harusi.

Mama wa watano ambaye alikuja Nairobi siku ya Ijumaa akizungumza kupitia video ya Instagram alisema kuwa atakuwa na harusi yake siku ya Nelson Mandela.

Image result for zari and king bae

Siku ya kusherehekea maisha ya Nelson Mandela ni Julai 18 ambayo ni wiki tatu kutoka sasa.

Kulingana na Zari, wao walichagua siku hiyo kwa sababu itakuwa siku nzuri ya kukumbuka ndoa yao kama ulimwengu utakumbuka Nelson Mandela kwa mazuri aliyefanya kwa Afrika.

Zari Hassan with King Bae

“Nipo karibu kuolewa na mimi na mpenzi wangu tunafikiria Siku ya Nelson Mandela kwa sababu itakuwa siku nzuri sana kukumbuka ndoa yetu kwa sababu Nelson Mandela alifanya mengi kwa ajili ya Afrika na si tu Afrika Kusini. Kwa hivyo mimi nitaolewa rasmi siku ya Nelson Mandela, “alisema.

Zari Hassan yupo Kenya kwa mkutano wa uwezeshaji wa wanawake uliopangwa na mwimbaji Akothee.

Kwa sasa, Zari ni mchumba wa Kingbae ambaye hajawahi kuonyesha uso wake na likuwa amesema harusi yao itakuwa ya kisiri ambapo familia na marafika wachache wataalikwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *