AFCON2019: Kenya yashinda derby ya Afrika Mashariki dhidi ya Tanzania

Image result for kenya beats tanzania afcon

Kombe la Mataifa ya Kiafrika, AFCON, mkanda wa soka mkubwa wa bara unaendelea nchini Misri. Ilianza Juni 21 baada ya sherehe ya ufunguzi.

Baada ya Kenya na Tanzia kushindwa kwa mechi za kwanza dhidi ya Algeria na Senegal mtawalia, jana wawili walipata kuonana kwenye mechi kali ya kujua timu gani inafunga virago na kwenda nyumbani.

Image result for kenya beats tanzania afcon

Kenya walijikakamua kushinda Tanzania na sasa wapo kwenye ngazi moja na Senegali ambao watakutana kwenye mechi ya mwisho wa kikundi.

Tanzania sasa itaonana na Algeria na kutathmini hatma yao kwenye AFCON ya mwaka wa 2019.

Kenya's forward Michael Olunga celebrates scoring his team's first goal during their 2019 Africa Cup of Nations match against Tanzania at the Stadium in Cairo on June 27, 2019. PHOTO | JAVIER SORIANO |
Michael Olunga akisherehekea bao lake la pili

Mechi ya jana ilikuwa Derby ya kwanza kabisa Afrika Mashariki na haijawahi tokea kwenye historia ya michuano ya bara ya Afrika.

Kwa sasa, Uganda na Kenya wapo katika fursa nzuri sana kuendelea kupanda ngazi wakielekea robo fainali.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *