Hongera! Eric Omondi awapiku wenzake kwa kuwa Mkenya mashuhuri mtandaoni baada ya Lupita Nyong’o

Image result for eric omondi

Eric Omondi yupo katika hali ya kusherehekea leo. Mfalme wa ucheshi amekwisha kufikia hali ya watu wa wa ngazi za juu nchini na wafuasi milioni 2 waliosajiliwa kwenye Instagram yake.

Eric amekaza kufikia aliko sasa na amepata mchango mkubwa kwenye Churchill Show na pia video zake za ajabu ambazo anazipachika kwenye Instagramu na Youtube.

Image result for eric omondi

Eric ametia bidii ili kufikia alipo sasa, kutoka kwa kusimamia masherehe, matukio, mikataba ya kukubaliana, matangazo ya bidhaa kama OLX na mengine mengi.

Kwa sasa, Eric Omondi alishinda tuzo la mcheshi bora barani Africa na kwa mwaka sasa amekuwa akijiita rais wa ucheshi Africa.

Licha ya kuvunjika moyo baada ya kuachana na msichana muitaliano, Chantal Grazioli, Omondi bado anaendelea kufanya kazi nzuri.

Image result for eric omondi coast

Ili kukujuza tu ni vipi Eric Omondi ameweza kupata wafuasi milioni mbili, haya ni baadhi ya vitu ambavyo amevifanya;

Mcheshi huyu ameunda urafiki na sehemu ya watu maarufu kwenye Afrika Mashariki. Kutoka kwa marais mpaka kwa wasanii, Eric Omondi sasa ni jina kubwa. Kwa leo tu, Msaani wa Bongo, Diamond Platinumz amempa pongezi na kumshukuru kwa kumpatia usaidizi wa kusambaza nyimbo zake.

Eric Omondi ametunga wimbo wa ucheshi wa ‘Kanyaga’ akiifuatia wimbo wa Diamond Platinumz.

Hii ni kumaanisha kuwa Eric Omondi anamfuata mwanamtindo Lupita Nyong’o mwenye ana wafuasi milioni saba (7). Lupita ni mwigizaji ambaye alijulikana saana baada ya filamu ya Wakanda iliyovuma.

Omondo amewapiku watu maarufu humu nchina kama msanii Bahati, Akothee, mtangazaji Jalang’o na DJ Mo, Huddah Monroe, Octopizzo.

Hawa ni baadhi ya wakenya ambao wameweza kufikisha wafuasi milioni moja kwenye mtandao wa Instagramu;

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *