Kikundi cha Ethic chamshirikisha mwanahabari Kamene Goro kwa wimbo mpya- Video

Image result for Ethic entertainment

Vijana wa kikundi cha Ethic wamerudi tena na mziki mpya ambayo imeleta mbwembwe kwenye mtandao.

Kikundi hicho ambacho kina vijana wanne, Swat, Rekles, Zilla na Seska wameshangaza wengi baada ya kumweka mwanahabari Kamene Goro kama mwanamtindo.

Vijana hao pia wanajulikana kwa wimbo wao wa kusisimua wa Lamba Lolo ilizindua mziki wa aina yake ya mitaani.

Video hiyo iliundwa na VJ One na mwanahabari Kamene Goro alikuwepo kwenye video hiyo akicheza mziki na vijana hao.

Ethic walisaini mkataba na AI Records mapema mwaka huu na walisema kuwa wanatumai wataboresha sanaa yao kwa fursa yao.

Image result for kamene goro

Nyimbo ya Figa ipo kwenye ukurusa wa YouTube na kwa sasa imefikia mashabiki wengi wanaupendo nyimbo hiyo.

Kamene Goro aliwafurahisha wengi kwa kujitokeza kuwasaidia vijana wanaochipuka.

Tazama video ya Figa;

https://www.youtube.com/watch?v=7R8fhgmSBYE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *