Jeff Koinange amwacha Rubadiri kinywa wazi baada ya kusema ‘Threesome’ hewani

post-feature-image

Mwanahabari mashuhuri Jeff Koinange amegonga vichwa vya habari baada ya kutaja neno lililoonekana kama ‘mwiko’ na wengi akisoma habari.

Mwanahabari huyo wa televisheni ya Citizen alikuwa anasoma taarifa ya mapacha wawili wa Kakamega ambao walijaajaa kwenye mitandao ya kijamii mwezi iliyopita.

Image result for kakamega twins

Chembechembe za DNA zilitoka wiki iliyopita na ikafahamika kwamba Sharon na Melvin ni mapacha kwa asilimia mia.

Akitangaza na mwenziwe Victoria Rubadiri, Jeff Koinange alimalizia taarifa yake akisema kuwa watatu hao, Melvin, Sharon na Melon watakuwa na ‘threesome’ ya kufana.

Image result for jeff koinange and victoria rubadiri

Kwenye kamusi ya Oxford, ‘Threesome’ ama ‘utatu’ ni kitu chochote kile ambacho kinafanywa na watu watatu kama vile kutembea, kukula na hata pia kusoma.

Hata hivyo, kwa maana nyingine ambayo imevuma sana mtandaoni ni kushiriki ngono mkiwa watu watatu. Mashabiki waliotazama taarifa hiyo wanasema kwamba neno hilo halikufaa kuongelewa televisheni.

https://twitter.com/MutuNne/status/1140565572016582656

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *