Makonda, ni furaha ipi hiyo aliyokupa Manula?

Na Ally Kamwe

PAUL MAKONDA. Naheshimu uchapakazi wako mkuu. Nathamini juhudi zako za kuitengeneza Dar es Salaam mpya.

Dar yenye usawa. Haki na yenye kujali wanyonge. Kama hawajakwambia naomba nikwambie leo, kina Mama huku mtaani wanajivunia sana uwepo wako.

Mwerevu mmoja aliwahi kusema, “Nafsi iliyofanikiwa ni ile iliyo katika dua ya Mwanamke.” Umefanikiwa sana RC wetu kwa utendaji wako.

Mbali na hayo, nina jambo moja nataka kukuuliza Mkuu.. Eti ni furaha ipi hiyo aliyokupa golikipa wa Simba, Aishi Manula?

Ni furaha ipi hiyo mkuu ambayo kila ukikaa inazidi kupanda na kukolea kwenye nafsi yako?

Kufungwa MABAO 4 na TP MAZEMBE? Kufungwa Mabao 4 kwenye mchezo ambao Simba walitolewa kwenye michuano ya AFRIKA?

Kusema alifanya kazi kubwa kiasi Aishi anastahili zawadi, kwa sisi wadau wa soka umetushangaza kidogo.

Labda pengine hufatilii sana soka. Lakini kama ni mwenye kufatilia, ulichokifanya ni kitendo cha ajabu sana.

Kumbuka Simba walitangulia kwa bao la Emmanuel Okwi pale Lubumbashi.. Aishi unaempongeza alitakiwa kulilinda lile bao na sio kuruhusu MABAO MANNE.

Aishi hakuwa shujaa. Hastahili kukumbukwa/kusifiwa/kupongezwa kwa lolote pale.
Angalau ungesimama na kusema unampongeza kwa mechi zote. Angalau ingefikirisha japo sio sana.

Lakini kuendelea kusimama kwenye majukwaa makubwa ya matukio makubwa ya kisoka na kuendelea kumsifia Manula kwa mechi ile dhidi ya Mazembe, unatushangaza mkuu.

Unatupa maswali mengi mno!

Kibaya zaidi ni pale ulipomwambia Spika wa Bunge asikuundike tume kutafuta wapi unatoa pesa.

Ukasisitiza kua ‘pesa ziko kwa wananchi wa mkoa wako wa Dar es Salaam’. Kweli?? Pesa zetu umezitumia kwa ajili ya furaha yako binafsi??? Kweli Mkuu?

Dar es Salaam tuna chama chetu cha mpira (DRFA), ingenufaika zaidi na hizo “pesa za wananchi” kuliko matumizi uliyoyafanya.

Dar hii ina lundo la watoto wenye vipaji visivyokua na muendelezo. Dar hii imefikia hatua yanafanyika mashindano bila hata kikombe kwa bingwa!

Kuna Ligi za Mikoa mkuu. Sidhani kama unajua timu zako zinaendeleaje huko?

Mkoa unakuhitaji sana. Jamii ya mpira hapa Dar inahitaji kuona ukijitoa na kusaidia kama unavyosaidia kwingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *