HESLB: Maombi ya Mkopo kuanza Juni 15

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inatarajia kufungua mfumowamaombi kwa njia ya mitandao kuanzia Juni 15 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru amesema mwisho wa kutuma maombi hayo utakuwa Agosti 15 mwaka huu.

Badru amewataka waombaji wa mikopo kuzingatia mwongozo wa kuomba mkopo ambao unataja sifa, vigezo na utaratibu wa kuwasilisha maombi ya mikopo elimu ya juu na kuwasaidia  kuandaa nyaraka muhimu.

“Uzoefu wetu unaonesha kuwa waombaji wengi hukimbilia kwenye mtandao na kujaza fomu za maombi wakati mwingine bila kusoma mwongozo. Mwaka huu tumetoa mwongozo huu kwanza ili wausome kwa wiki takribani mbili kabla ya kuruhusiwa kuanza kujaza fomu kwa njia ya mtandao,” alisema.

Amesema, wameandaa kitabu cha lugha ya Kiswahili chenye maswali na majibu yanayoelekeza namna ya kuomba ambacho kinapatikana kwenye tovuti ya Heslb.

Badru ameongeza kuwa, waombaji wote wanatakiwa na vyeti vya kuzaliwa ambavyo vimethibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA). Aidha, kwa waombaji mikopo ambao wazazi wao wamefariki dunia, watatakiwa kuwa na nakala za vyeti vya vifo ambavyo vimethibitishwa na RITA au ZCSRA.

Kwa wanafunzi waliofadhiliwa na taasisi mbalimbali katika masomo yao ya sekondari au stashahada, hawa wanatakiwa kuwa na barua kutoka katika taasisi hizo,” amesema Badru katika mkutano huo uliohudhuriwa na Mkurugenzi wa Upangaji Mikopo wa HESLB

Kwa wanafunzi wenye ulemavu au wenye wazazi wenye ulemavu, Badru amesema wanapaswa kuwa na barua zinazothibitisha ulemavu wao kutoka kwa waganga wakuu wa wilaya au mikoa.

umri wa waombaji mikopo umeongezeka kutoka miaka 33 hadi 35 na wanafunzi waliomaliza kidato cha sita au stashahada ndani ya miaka mitano iliyopita wanaruhusiwa kuomba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *