Zamaradi Mketema: Kwangu umekuwa vyote, Mume na Baba wa watoto wangu

Zamaradi, mumewe na watoto wake

Mwanadada mhamasishaji maarufu wa masuala mbalimbali ya kijamii kupitia mtandaoni nchini Tanzania, Zamaradi Mketema amesema kwamba mwanamke anaweza kupata baba mzuri kwa watoto lakini asiwe mwanaume mzuri kwa mkewe na vivyo kupata mwanaume mzuri lakini asiwe baba mzuri.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Zamaradi ambaye pia amewahi kuwa mtangazaji wa kituo cha Clouds ameandika maneno hayo huku akihusisanisha na mumewe ambapo amemsifu kwa kuwa baba mwema kwa watoto wake na mwanaume mzuri kwake pia.

 

View this post on Instagram

 

Unaweza bahatika kupata BABA mzuri kwa watoto lakini asiwe mume/mwanaume mzuri kwako, na unaweza kupata Mume/Mwanaume anaekupendeza ila akashindwa kuwa Baba unaemtaka kwa watoto, ASANTE MUNGU kwa kunipa mtu sahihi kwa wakati sahihi. Kwangu Umekuwa Vyote, Mume na Baba wa watoto wangu, lakini zaidi MLINZI na kama mzazi kwangu, kuna muda unakuwa Protective mpaka naweza kuchukia but i know its just Love, and I love you more… Asante MUNGU kwa ajili ya wewe kwenye maisha yangu, umekuja sio tu na Baraka nyingi, ila umeniletea Furaha na Amani kubwa ya moyo, Asante kwa kunifanya MALKIA kwenye Ufalme wako, I always feel safe in your Hands, nataka tu ufahamu Nakupenda na kukuthamini sana, I will never take you for Granted, na wala sitatake advantage ya Upendo wako uliopitiliza kwangu, Kuna muda naona MUNGU amenipendelea kunipa wewe, sitataka kumuangusha kwa kutoithamini zawadi hii, Nakupenda Mume wangu @smsgarage_tz #Myfullpackage #HeavenSent

A post shared by zamaradi mketema (@zamaradimketema) on

“Unaweza bahatika kupata BABA mzuri kwa watoto lakini asiwe mume/mwanaume mzuri kwako, na unaweza kupata Mume/Mwanaume anaekupendeza ila akashindwa kuwa Baba unaemtaka kwa watoto, ASANTE MUNGU kwa kunipa mtu sahihi kwa wakati sahihi,” ameandika Zamaradi.

“Kwangu Umekuwa Vyote, Mume na Baba wa watoto wangu, lakini zaidi MLINZI na kama mzazi kwangu, kuna muda unakuwa Protective mpaka naweza kuchukia but i know its just Love, and I love you more.”

Zamaradi ambaye pia mzazi mwenza na aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media marehemu Ruge Mutahaba amemshukuru Mungu kwa kumjaalia mume ambaye amekuwa ni furaha kubwa na amani ya moyo wake na zaidi kumfanya kuwa Malkia kwenye ufalme wake.

” Asante MUNGU kwa ajili ya wewe kwenye maisha yangu, umekuja sio tu na Baraka nyingi, ila umeniletea Furaha na Amani kubwa ya moyo, Asante kwa kunifanya MALKIA kwenye Ufalme wako, I always feel safe in your Hands, nataka tu ufahamu Nakupenda na kukuthamini sana.”

“I will never take you for Granted, na wala sitatake advantage ya Upendo wako uliopitiliza kwangu, Kuna muda naona MUNGU amenipendelea kunipa wewe, sitataka kumuangusha kwa kutoithamini zawadi hii, Nakupenda Mume wangu.”

 

View this post on Instagram

 

Sundaying’ ❤️

A post shared by zamaradi mketema (@zamaradimketema) on

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *