Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka wananchi kua makini na taarifa za uvumi zinazoendelea kuhusu mikopo inayotolewa na WEKEZA SACCOSS ikimuhusisha yeye.
Waziri Ummy aliandika katika ukurasa wake wa mitandao ya kijamii wa Instagram na Twitter na kufafanua kwamba hausiki na Mikopo yoyote inayodaiwa kutolewa na WEKEZA SACCO’S au Taasisi nyingine yoyote.
Wazir Ummy ameliomba Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali wote wanaofanya udanganyifu huo.
Posti ya mtandao wa kijamii wa twitter ya Waziri Ummy Mwalimu ikionyesha taarifa inayosambaa ikidai anahusika na mikopo hii hapa:
Wananchi kuweni makini. Sihusiki na Mikopo yoyote inayodaiwa kutolewa na WEKEZA SACCO’S au Taasisi nyingine yoyote. Nimeliomba Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali wote wanaofanya udanganyifu huu pic.twitter.com/BuYgWG8N5D
— Ummy Mwalimu, MP (@umwalimu) June 2, 2019
Aidha, tabia hizi za utapeli si mara ya kwanza kwani jina la Mke wa Rais John Magufuli, Mama Janeth Magufuli lilishawahi kutumika katika akaunti ya mtandao wa kijamii wa Facebook kudanganya watu waombe mikopo.
Kufuatia hali hiyo Msemaji wa mkuu wa serikali alitahadharisha wananchi kuipuuzia akaunti hiyo May 30 mwaka huu kupitia akaunti ya tweeter isome hapa chini
Akaunti hii ni feki, ipuuzwe.Mamlaka husika zinachukua hatua kali. Tafadhali epuka kujihusisha nayo. pic.twitter.com/UCvJdwXbQX
— Msemaji Mkuu wa Serikali (@TZMsemajiMkuu) May 30, 2019