Unamkumbuka Mzee Magali wa Bongo Movie? Leo amekuja na stori mpya kabisa

Unamkumbuka yule mcheza filamu mkongwe wa Bongo Movie, Charles Magali? Sasa ni hivi ameibuka na kuweka hadharani siri ambayo kwa muda mrefu alikuwa amekaa nayo moyoni tangu wakati yupo mtoto ambapo amesema kuwa aliwahi kumuwekea mwalimu wake upupu kwenye kiti chake.

Mzee Magali amesema kuwa katika kipindi chake cha utoto mpaka ujana alikuwa mtemi sana na tukio kubwa analolikumbuka ni pale ambapo alipokuwa na ugomvi na wanafunzi wenzake halafu baadaye mwalimu kuingilia na kumpa adhabu ya viboko na kukasirishwa hali iliyosababisha kumkomesha mwalimu huyo kwa kumwekea upupu.

“Nilipotandikwa na mwalimu nilikasirika sana, siku iliyofuata nilisaka upupu na kumuwekea kwenye kiti chake, bila kujua alikikalia akakiona cha moto, kwani alijikuna mpaka akajibandua ngozi, alibaini kuwa ni mimi ndio nilifanya hivyo akahamishia soo nyumbani,” Mzee MAGALI ameiambia Ijumaa Wikienda.

Baada ya kesi hiyo kupelekwa nyumbani, baba wa Magali ambaye alikuwa mkali sana aliamua kumuadhibu hali iliyomfanya aamue kuhama nyumba hadi hasira za baba yake zilipoisha ndipo akarudi.

Mzee Magali ni moja ya waigizaji wakongwe na bora kuwahi kutokea nchini Tanzania kutokana na umakini wake katika kuigiza kwenye kila aina ya uhusika ambao amekuwa akiwekwa.
Ameigiza filamu nyingi sana hasa na marehemu Steven Kanumba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *