Mume na mke wahukumiwa kulipa faini ya Sh milion 20 kwa kuajiri raia wa nje bila kibali

Mkurugenzi wa kampuni ya Biabana, Anna Kristina Edler, (54) na mumewake,
Anders Svensson 58 wamehukumiwa kulipa faini ya sh. Milioni 20 au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu gerezani baada ya kukiri tuhuma za kuajiri raia wa nje ya nchi na kujihusisha na kazi bila ya kuwa na kibali nchini

Hukumu hiyo imesomwa, leo Juni 3,2019 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo washtakiwa hao raia wa Swideni wanakabiliwa na mashtaka mawili, likiwemo La kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali.

Baada ya kusomewa mashtaka yao, washtakiwa wamekiri kutenda kosa hilo, na wamehukumiwa kulipa faini ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu gerezani.

Mapema akisoma mashtaka yao, wakili wa serikali, Daisy Makakala amedai kati ya Agosti 18 mwaka Jana na Aprili 3, 2019 huko Mikocheni, mshtakiwa Elder, akiwa kama mkurugenzi wa kampuni ya Biabana Ltd alimuajiri Anders na kufanya kazi Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka idara ya Uhamiaji.

Katika shtaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo mshtakiwa Enders alijihusisha na kazi kama muajiriwa wa kampuni ya Biabana LTD bila ya kuwa na kibali kinachotolewa na idara ya Uhamiaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *