MAONI YA WABONGO MTANDAONI BAADA YA RAISI MAGUFULI KUKUTANA NA GWAJIMA IKULU LEO!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dk Josepaht Gwajima Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akutana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Na kama ilivyoada kwa wageni wanaomtembelea rais Magufuli ikulu hutoka na kuzungumza mbele ya waandishi maalumu wa ikulu,na kwa upande wake askofu Gwajima amempongeza  rais Magufuli kwa kuamua kujenga mradi wa kufua umeme wa Stigler’s Gorge na kuwatoa wasiwasi watanzania juu ya mradi huo na yanayosemwa na mataifa ya nje.

 

Kama ilivyoada ya wananchi wa mtandaoni (Netizens) wa Tanzania wakaingia katika viwanja mbalimbali iliyopostiwa stori hiyo na kucomment ikumbukwe kuwa mwanzoni mwa mwezi wa nne Askofu Gwajima alikumbwa na kashfa ya video ya ngono iliyosambaa mitandaoni ambayo polisi walikana juu ya video hiyo kuwa ni ya askofu huyo.

Haya hapa baadhi ya maoni ya watanzania mtandaoni juu ya Askofu Gwajima na alichokiongea leo mbele ya Kamera baada ya kukutana na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli.

Huyu hapa jumbejr_tz  yeye kaandika “kwani hao watu wa magharibi huo mradi upo kwao au kwetu?.hao watu wa magharibi wanataka kutuburuza ila kwa sasa wamenawa hatutaki sisi tunataka maendeleo”

 

Katika mtandao wa Instagram kwenye post ya Milard Ayo kuna mdau aitwae joshma_desh   yeye ameandika“Askofu kaongea point Kali Sana. Kwamba ili tuwe na maendeleo kuna watu na mipango yao imeharibiwa zaidi ktk mradi huu wa Stigler’s George 😂😂😂.heshima kwako JPM”

Wapo pia walioweka utani kama khalid.msangi.94 “nikianglia mkono siyo wake niwa baunsa” comment hii inahusiana na utetezi alioutoa Askofu huyo wakati akikanusha juu ya video ya ngono iliyokua inasambaa mtandaoni kwa kusema video ile ilihaririwa na kuongeza kuwa hata mikono sio yake ni ya baunsa.

Na pia mtumiaji mwenye jina la djcavanni kaandika . kwa kuuliza swali “@millardayo ivi muheshimiwa Rais atakuwa amebahatika kuona zile clip walizomuedit ndugu mchungaji eeh ?? 

Nae din_kush  kaandika “Ni wivu tu.. Ni wivu tu 😂😂😂”

 

Kufuatia comments nyingi kuwa zile za utani kwa Askofu Gwajima wakihusisha na video ile ya ngono  baadhi ya wananchi mtandaoni wamekasirishwa na comments hizo na kuandika  daudicretus “Kuna watu bhana vituko sana,, wanakuwa speed kwenye mambo ya kipuuzi na kuwa slow kwenye mambo ya faida, yan siku mmezidi hata nafasi ya Mungu kwa kuwa wahukumu,. Kinacho ongelewa leo hapo ni mambo ya umeme, ww umeanza kuleta mambo ya mange mara video,, huoni kama una akili chafu ww”

Napo kwenye mtandao wa  Jamii Forum mtumiaji mwenye jina la Carter  “ameandika Labda wawekezaji wapya…vichwa vya jongoo. Kuna Yule mtumishi alisema serikali ya JPM ikiweza kujenga SGR yeye atanunua vichwa vya treni. Ahadi ni deni”

Maoni haya ya “Carter” yanatokana na ahadi aliyotoa mchungaji huyo miaka miwili iliyopita kuwa amedhamiria kununua treni ya umeme baada ya Rais John Magufuli kuonyesha dhamira ya kujenga reli ya kisasa(standard gauge).

 

Je na wewe una maoni juu ya ugeni huu wa mheshimiwa Rais ikulu leo basi usisite kutuandikia hapo chini!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *