Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe amempongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba kutokana na utekelezaji wake wa majukumu.
Kabwe aliandika hayo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter ambapo amesema, ni siku ya pili tu lakini kuna tofauti kubwa ya namna ya utekelezaji anaoufanya Makamba.
Mbali na hayo, Zitto ameushutumu utendaji wa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kutokana na umaskini wa wavuvi na kudai kwamba angekua na utendaji kama wa Makamba kusingekua na umaskini.
Tazama Tweets za Zitto hapa chini:
Siku ya Pili tangu marufuku ya plastiki ianze, unaweza kuona tofauti kubwa miongoni mwa Waziri wa Serikali moja katika kutekeleza masuala. Hebu fikiria kama Luhaga Mpina angefanya alichofanya @JMakamba kuna mvuvi angelia kutiwa umasikini? @Kokunuranalisa ulikuwa sahihi bana
— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) June 2, 2019
Some positive news from Tanzania to the world after so long time https://t.co/sxzGqXLlVZ Tanzania bans plastic bags to clean up environment. Congratulations to @SuluhuSamia and @JMakamba for the leadership on this.
— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) June 2, 2019