Waziri Mkuu: Wanaodai korosho kulipwa mwaka huu wa fedha

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa, amesema wakulima ambao hawajalipwa malipo ya korosha serikali itaanza kulipa fedha hizo mwaka huu wa fedha ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 20.

Alisema baada ya serikali kukamilisha uhakiki wa majina kwa wale wakulima ambao hawajalipwa yatawasilishwa katika Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa ajili ya malipo.

“Mwaka huu wa fedha malipo yao ya korosho watalipwa ni haki yao na serikali haipo tayari kumdhulumu mkulima yoyote katika kupata haki yake,” alisema Majaliwa.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani katika kikao cha Halmashauri Kuu ya mkoa CCM, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, alieleza kuwa ulipaji wa korosha unaendelea.

Alisema hadi Mei 31 mwaka huu zaidi ya kilo milioni 51.99 zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 171.57 sawa na asilimia 87.6 zimeshalipwa kwa wakulima husika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *