Waziri Jafo atoa agizo kwa Halmashauri

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo ameziagiza Halmashauri zihakikishe zinakua na shule za kidato cha tano hususani masomo ya sayansi na hisabati kufikia Machi 2020.

Wazir Jafo ameyasema hayo mjini Dodoma wakati akitangaza kuhusu orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi kwa mwaka wa masomo utakao anza mapema mwezi Julai, 2019.

Amezitaja halmashauri hizo kuwa ni pamoja na Kyerwa Mkoani Kagera, Kilindi na Handeni Mkoani Tanga, Kilombero na Malinyi Mkoani Morogoro, Mtwara DC, Momba Mkoani Songwe, pamoja na Nanyumbu Mtwara.

Shule zitakazoanzishwa lazima ziwe na maabara ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa masomo ya sayansi ambao ufaulu wao umekua ukiongezeka kila mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *