Mifuko mbadala yawa dili kupatikana

Ikiwa leo ni siku ya kuanza matumizi ya mifuko mbadala, bidhaa hiyo imekuwa ni changamoto kuipata katika masoko na kusababisha wafanyabishara kugombania.

Baadhi ya wanunuzi ambao wanakwenda kuiuza madukani na wale wanaokwenda kuweka dukani kwa ajili ya kuwafungashia bidhaa wateja wao, walisema tangu juzi bidhaa hiyo ni shida kuipata.

Walisema kuwa awali mifuko ya ujazo wa kilogram tano ilikuwa ikipatikana kwa gharama ya Sh. 300 lakini bidhaa hiyo jana ilipatikana kwa wafanyabiashara wachache kwa Sh. 350.

Naye Abdallah Juma ambaye ni mfanyabiasha alisema leo mifuko mbadala inapatikani kwa shida kutoka kwa wafanyabiashara wachache na wengine wameinunua na kuiuza kwa bei ya juu.

Hamisa Omary alisema upatikanaji wa mifuko hiyo ni changamoto kwani wanauziwa gharama kubwa kwa ile yenye ujazo wa kilogram tano.

“Kama unavyoniona hapa nimenunua kwa wauzaji wa jumla wa hapa Kariakoo na mimi nauzia wanunuaji wa jumla wanaotoka maduka mengine kwa Sh. 350 angalau napata na mimi Sh. 50 kama faida yangu,” alisema.

Katibu wa Umoja wa Wafanyabishara wa Mifuko Mbadala katika soko la Karikakoo, Ramadhani Mussa, alisema bidhaa hiyo haitoshelezi kulingana na mahitaji ya soko.

Mussa alisema wauzaji wa jumla wa mifuko hiyo mbadala wanapokea asilimia 15 ya bidhaa zote zinazozalishwa viwandani na wao kuuza kwa wanunuzi na wafanyabishara wengine.

Alisema sababu za uzalishaji huo kuwa mdogo ni kutokana na wenye viwanda kuwa na mashine chache, hivyo zitakapoongezeka changamoto hiyo itakwisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *