Wizara ya Fedha yapata mabilioni ya fedha

Serikali kupitia  wizara ya fedha Tanzania imepokea mali zilizotaifishwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza zikiwamo fedha na dhahabu zaidi ya kilo 325 yenye thamani ya zaidi ya Sh27 bilioni zilizokamatwa Geita zikitoroshwa na wafanyabiashara wakishirikiana na askari polisi.

Vitu vingine vilivyotaifishwa ni pamoja shilingi milioni 305 ziliandaliwa kwa ajili ya kuwahonga maafisa,  na mizani ya kupimia madini pamoja na mashine ya kupima ubora wa thamani ya madini.

Fedha hizo zilikabidhiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga ambae amesema amechukua hatua hiyo kutokana na washtakiwa wanne waliohukumiwa kifungo au faini kutokata rufaa.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Khatibu Kazungu  akiri kupokea vitu vyote hivyo

“Nakiri kupokea dhahabu kilo 325, pamoja na fedha taslimu milioni 305,  na nimeongea na waziri wa fedha asubuhi, ameniambia hizo fedha anazihitaji sana kwa ajili ya kufanikisha na kugharamia huduma mbalimbali za kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *