UKWELI KUHUSU WANAUME WENGI KUUGUA MARADHI YA AKILI

Maradhi ya akili hujumuisha matatizo mengi tofauti tofauti, takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonyesha, mtu mmoja kati ya watu wanne ana hatari ya kusumbuliwa na maradhi ya akili. Kuna takriban watu Milioni 450 ulimwenguni kote wenye maradhi ya akili.

Takwimu za mwaka 2014 zinaonyesha jumla ya wagonjwa 10,000 wamehudumiwa katika Hospitali ya Taifa ya Tanzania ya Muhimbili na wengine 2,000 kulazwa katika kipindi kutokana na maradhi ya akili.

Wakati takwimu hizo za shirika la Afya duniani na Hospitali ya Muhimbili zikionyesha hivyo, watu wengi wanaamini kuwa idadi ya wanaume wanaougua maradhi ya akili ni kubwa kuliko wanawake kutokana na uwingi wao m licha ya hali halisi kuwa kinyume na imani hizo.

Frank Masao daktari bingwa wa magonjwa ya akili kutoka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anaelezea ukweli kuhusu uwiano wa magonjwa ya akili kati ya wanaume na wanawake.

Anasema wanaume wengi wanafikishwa hospitalini hapo kwa tatizo la maradhi ya akili kuliko wanawake kutokana na tabia hatarishi wanazozionyesha mara wapatapo ugonjwa huo.

Anasema, mwanaume akiugua ugonjwa wa akili anakuwa na tabia hatarishi nyingi zaidi kuliko mwanamke, anaweza akapiga, akawa mkali, akatukana, akavunja na akatumia silaha hali inayoilazimu jamii kumuwahisha hospitali kutokana na kushindwa kumdhibiti.

“Hii ni tofauti kwa wanawake wengi ambao hawana tabia hatarishi kama wanaume, hawapigi, hawatukani, hawavunji, hawatumii silaha, hawatishii na hata wale wachache wanaofanya tabia hizo ni rahisi kuwadhibiti,”

“Tofauti katika tabia hatarishi zinaifanya jamii iseme kwamba wanaume wenye matatizo ya akili ni wengi kuliko wanawake, kimsingi wote wana uwiano sawa katika kuugua lakini wanaoletwa hospitali zaidi ni wanaume kutokana na tabia hatarishi,” alisema Dk. Masao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *