MO Dewji akata mzizi wa fitna usajili wa Ajibu Simba

Mwekezaji ndani ya klabu ya Simba Mohamed Dewji ‘Mo’ ameizungumzia ishu ya Ibrahim Ajibu kuhusishwa kurejea Msimbazi.

Mo Dewji amesema kwa sasa bado hawajaanza mazungumoz na mchezaji yeyote kutoka nje na ndani ya Simba na wakiwa tayari kila kitu kitawekwa wazi.

“Kiukweli hili jambo bado hatujakaa wala kumaliza, kwahiyo kwa muda wa wiki nzima tutakaa na tutaona, kwa nini hujasikia hadi leo John Bocco au wachezaji wengine wamesaini kwa hiyo hadi sasa bado hatujasaini wachezaji.”
.
“Mungu akitujalia siku zijazo tutajua tu,” amesema Mo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *