Makonda amwaga mamilioni washindi tuzo za ‘Simba Mo Awards’

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila mchezaji wa Simba ambaye ameshinda tuzo za ‘SIMBA MO AWARDS’ huu mlinda lango Aishi Manula akilamba milioni kumi kwa kushinda tuzo ya kipa bora.

Makonda ameahidi zawadi hizo wakati hafla ya ugawaji tuzo za “Simba Mo Awards” usiku wa jana ambapo ametoa kiasi kikubwa zaidi kwa Manula kutokana na kazi kubwa aliyoifanya katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ambapo hata hivyo Simba waliondoshwa kwa wastani wa mabao 4-1.

“Naahidi ktoa milioni moja kwa kila mchezaji wa Simba SC atakayeshinda tuzo leo (jana) na vile vile nitamzawadia milioni kumi Aishi Manula kutokana na kiwango alichokionesha katika mchezo dhidi ya TP Mazembe Lubumbashi,” amesema Makonda.

Tuzo za ‘Simba Mo Awards’ zimeanza rasmi msimu uliopita ambapo muasisi wake Mohamed Dewji ambaye ni mwekezaji wa klabu hiyo ameanzisha tuzo hizo maalum kwaajili ya kuwapa wachezaji motisha ya kufanya vizuri zaidi kila msimu mpya unapoingia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *