Kuwa Diamond Plutnumz ni mara moja tu!

Nyota wa muziki mkali zaidi kwa sasa nchini Tanzania Diamond Plutnumz amesema anataka kuwa Diamond wa kwanza (first Diamond) na si vinginevyo.

Kupitia video iliyopo kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram, Diamond amesema hayo wakati akitolea mfano wa muigizaji nguli wa ngumi kutoka nchini Uchina Jackie Chan wakati alipoulizwa kama angependa kuwa Bruce Lee ambapo alijibu kwamba anataka kuwa Jackie Chan wa kwanza (first Jackie Chan).

“Niliona siku moja alihojiwa Jackie Chan akaulizwa would you like to be next Bruce Lee (ungependa kuwa Bruce Lee ajaye), akasema I don’t want to be the next Bruce Lee (sitaki kuwa Bruce Lee ajaye), I want to be the first Jackie Chan (nataka kuwa Jack Chan halisi), so I want to be the first Diamond (nataka kuwa Diamond halisi) na sio mtu mwingine yeyote.”

Kauli hii ameitoa kama namna ya kutoa hamasa kwa mashabiki wake na muziki kwa jumla kuhudhuria kwenye tamasha lake la muziki litakalofanyika Mjini Kahama siku ya Idd Mosi.

Amesema kwa kuzingatia mtazamo chanya ktakachoweza kufanikisha yeye kuwa hivyo ni kufanya kitu kilicho bora kama vile kutumbuiza vyema jukwaani ambapo kunaweza kukufanya mtu akupende zaidi au akuchukuie, aupende wimbo au auchukie.

Amesema ukiwa unaweza kutumia jukwaa vizuri inafanya nyimbo zake zipendwe zaidi.

Diamond ni moja ya wasanii wanaopendwa zaidi kwa sasa nchini Tanzani na Afrika Mashariki kutokana na ngoma zake kali anazotoa mara kwa mara.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *