APR wakisanua usajili wa Bigirimana Yanga

Kufuatia klabu ya Yanga kutangaza kumsajili nyota kutoka APR ya Rwanda Issa Birigimana, Katibu Mkuu wa Klabu ya APR Adolphe Kalisa, amesema ameshangazwa na taarifa hizo kwani mchezaji huyo bado ni mali yao halali.

Kalisa ameeleza kuwa ni jambo la kushangaza kuona klabu kubwa kama Yanga ambayo anaamini imejaa watu wenye weledi kufanya jambo kama hilo bila kufuata taratibu zinazostahili ilhali mchezaji huyo bado ana mkataba na APR.

Tayari uongozi wa klabu ya Yangakupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Federick Mwakalebela umeshatangaza kuwa Bigirimana ni mchezaji wa Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili utakaomalizika mwaka 2021.

“Tumeishangaa klabu kubwa Kama Yanga kumsajili mchezaji wetu Issa Birigimana ambaye bado ana mkataba mpaka 2020.

“Hatuna uhakika kama klabu hii ina katibu mkuu, hatua za kisheria zitafuata.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *