Wanne wa kigeni, watatu wazawa panga linawahusu Simba

Taarifa kutoka klabu ya Simba zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Simba uko mbioni kuwatoa kwa mkopo wachezaji watatu akiwemo mshambulizi Adam Salamba kwaaili ya kuwapa uzoefu zaidi katika siku zijazo.
Salamba ambaye alisajiliwa na Simba msimu huu akitokea Lipuli FC ya Iringa kwa dau la Sh milioni 40 inaelezwa pia yuko mbioni kuelekea nchini ureno kwaajli ya kusakata kabumbu.
Mshambulizi huyo amekuwa hana namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Simba kilicho chini ya kocha Mbelgiji Patrick Aussems kutokana na kujaa wachezaji wenye ushindani mkubwa katika nafasi yake. Wachezaji kama Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi, wamekuwa ndiyo sababu kubwa ya Salamba kusugua benchi.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa wachezaji wengine ambao wanatarajiwa kutolewa kwa mkopo ni Rashid Mohammed, anayetarajiwa kupelekwa nchini Kenya na Abdul Mohammed, ambaye haijajulikana atakwenda timu gani.

                                   Adam Salamba ni moja ya wachezaji wanasemekana kutolewa kwa mkopo

Aidha, chanzo hicho kilieleza kwamba, tayari Aussems amekabidhi ripoti yake kwa uongozi inayoonyesha wachezaji watakaoachwa lakini hakuwataja kwa majina.
Hata hivyo, mtoa taarifa huyo alisema alichoeleza kocha ni kwamba wataachwa wachezaji wanne wa kigeni na watatu wazawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *