PUTIN AWASILISHA BUNGENI MUSWADA WA KUJITOA KATIKA MKATABA WA INF NA MAREKANI

Mfumo wa kurushia makombora wa Iskander-M na 9M729 , ambayo Marekani inaishutumu Urusi kwa kuvunja  mkataba wa INF.

Raisi wa urusi Vladmir Putin leo amewsilisha muswada katika bunge la nchi hiyo (Duma) wa kujitoa katika mkataba wa INF baina yake na Marekani, tayari Marekani inatarajiwa kujitoa ndani ya mkataba huo ifikapo Agostit mwaka huu.

Mwezi wa pili mwaka huu Marekani ilitangaza kujiondoa katika mkataba huo baada ya kuilaumu Urusi kwa kukiuka makubalino ya mkataba huo baada ya kufanya majaribio ya mfumo wake wa kurusha makombora wa Iskander na 9M729.

Tayari bunge la Urusi linatarajia kupitisha muswada huo alhamis hii na Putin ataweza kupitia na kuamua kujitoa katika umja huo akipenda.

INF ni nini?

Ni mkataba uliosainiwa kati ya Marekani na Umoja wa nchi za Kisoviet mwaka 1987

Mkataba huu unazipiga marufuku Urusi na Marekani kutengeneza mitambo ya kurushia makombora ya masafa ya ardhini yatakayowez kupiga kuanzia kilomita 500 hadi 5500.

Makubaliano hayo yaliingiwa ili kuondoa hali ya uhasama iliyokuwepo katika nchi za Ulaya ,ambapo nchi zote zilikua na mifumo ya kurushia mkombora hayo yenye uwezo wa kupiga kilomita 500 hadi 5500

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *