Mambo makubwa matano ya kufahamu baada ya Chelsea kuifunga Arsenal 4-1 Europa League

Usiku wa kuamkia leo kulikuwa na Fainali ya Michuano ya Ligi ya Europa ambapo Chelsea walikuwa wakikabiliana na Arsenal, timu zote hizi zikitoka nchini England.

Katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Baku Olympic huko nchini Azerbaijan, Chelsea wameibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya mahasimu wao wa jiji la London Arsenal. Magoli ya Chelsea yamefungwa na Oliver Giroud (49), Pedro Rodriguez (60), Eden Hazard (65 penati na 72) huku bao la kufutia machozi la Arsenal likifungwa na Alex Iwobi dakika ya 69.

Mambo matano unayopaswa kujua kuhusu mcheo huo

  • Cheslsea wameshinda  fainali yao ya nne katika michuano ya vilabu ngazi ya Ulaya, wakizidiwa na Liverpool ambao wameshinda mara nyingi zaidi kwa vilabu vya England (mara nane)
  • Arsenal wameruhusu mabao manne katika michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mara ya mwisho walipofungwa 5-1 na Bayern Munich Machi 2017 na ni timu ya kwanza kupoteza kwa wastani wa magoli mengi kwenye michuano ya Ligi ya Uropa tangu ilipotokea kwa Middlesbrough walipofungwa mabao 4-0 na Sevilla mwaka 2006.
  • Chelsea imekuwa timu ya kwanza kushinda taji kubwa la Ulaya bila kupoteza hata mchezo mmoja (ushindi mara 12, Sare mara 3) tangu ilipotokea hivyo kwa Manchester United 2007-08 kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
  • Arsenal wamepoteza fainali kubwa tano kati ya sita zinazosimamiwa na UEFA, zikijumuishwa na zile tano za mwisho mfululizo (1995 Cup Winners’ Cup, 2000 Uefa Cup, 2006 Champions League, 2019 Europa League)
  • Chelsea wameshinda mechi 12 za Ligi ya Europa kwa msimu wa 2018-19. Timu pekee kufanya zaidi ya hivyo kwenye michuano ya Ulaya kwa msimu mmoja ni Atletico Madrid msimu wa 2011-12, ambapo walishinda mechi 13.
  • Hazard ameaga rasmi kwamba anaondoka

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *