Maalim Seif: Sitawaangusha Wazanzibari

Mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za visiwani Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewaahidi wazanzibar kurudisha imani na mapenzi yao kutokana na kumuonyesha imani na mapenzi makubwa katika kipindi chote ambacho amekua akiwaongoza katika mapambano yenye kuleta mabadiliko.

Maalim seif ameyaandika hayo katika ukurasa wake wa twitter kufuatia ziara yake ya kutembelea Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa dhumunii la kuwaangalia na kuwafariji wagonjwa, wafiwa na wazee mbali mbali.

Maalim Seif huwatembelea wagonjwa, wafiwa na wazee kila ifikapo mwezi wa Ramadhani na amekua akifanya hivyo kwa miaka mingi sasa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *