Kipindupindu Tishio Dar, Wanaotiririsha maji machafu kuisoma namba

Watu 32 wamefikishwa hospitalini kutokana na ugonjwa wa kipindu pindu jijini Dar es Salaam ambapo hospitali ya Temeke ikiongoza kwa idadi kwa kua na wagonjwa 18, Amana wagonjwa 13 huku hospitali ya mwananyamala ikiwa na mgonjwa mmoja.

Kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewataka wananchi wa Dar es salaam kujihadhari na janga hilo kwa kuacha kutiririsha maji machafu mitaani hasakatika kipindi hichi cha mvua.

Aidha, amezitaka manispaa za Dar es salaam kuweka faini kubwa kwa wote wanaotiririsha maji machafu mitaani na kutoa rai kwa wananchi kuwaripoti watu hao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *