Waandishi Wamtaka Mkuu wa Mkoa Awaombe Radhi.

Umoja wa waandishi wa  Habari Mkoani Iringa umempa  siku saba Mkuu wa Mkoa huo, Ally Hapi kuwaomba radhi baada ya kuwataka nao kuwa na vitambulisho vya Wafanyabiashara wadogo

RC Hapi alitoa kauli hiyo juzi Jumatatu Mei 27, 2019 wakati akizungumza na watendaji wa Serikali kuhusu ugawaji wa vitambulisho vya Wafanyabiashara ambapo aliwataja Waandishi wa habari kama Wafanyabiashara na vibarua wasio rasmi

Alisema “Wafanyabiashara ni wengi kuna wapiga debe, wauza nyanya, mchicha, wachoma mahindi na hata Waandishi wa habari na wapiga picha wote wanatakiwa kuwa na vitambulisho ili kuchangia kodi kutokana na kazi wanazofanya.”

Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Iringa, Frank Leornald amesema kauli ya RC Hapi inadhalilisha taaluma ya habari, hivyo wamefanya majadiliano na kuazimia mambo sita watakayoyawasilisha kwa RC Hapi wakimtaka kutoa tafsiri rasmi anayoijua yeye kuhusu waandishi rasmi na wasio rasmi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *