SERIKALI KUAJIRI WATUMISHI WAPYA 44,800 BILA KUJALI UZOEFU

Watumishi 44,800 wenye sifa na vigezo wataajiriwa katika taasisi mbalimbali za serikali katika kipindi cha mwaka 2019/2020.

Hayo  yameelezwa na naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Dk Mary Mwanjelwa wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Aida Khenan aliyehoji kama kuna utaratibu wowote wa kuajiri watu waliohitimu vyuo na kukidhi vigezo vya kuajiriwa.

Katika swali la nyongeza mbunge huyo amehoji kwa nini Serikali inaendelea kuweka vigezo vya uzoefu kazini wakati inajua hakuna vijana wenye uzoefu. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama alijibu swali hilo kwa kusema kua wameondoa uzoefu badala yake Serikali imeanzisha kozi maalum kwa wahitimu ambazo husaidia kuwapa ujuzi.

Kwa sasa Bunge linaendelea Bungeni jijini Dodoma ambapo Mawaziri mbalimbali wameendelea kuwasilisha makadirio yao ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *