MKE AFANYA MAUAJI YA KUTISHA MOROGORO

Mkazi wa morogoro ameuliwa na mkewe kwa akishilikiana na watu wawili akiwemo mtoto wake kwa kupigwa na kitu kizito kichwani kwa madai ya wivu wa mapenzi.

Akizungumzia tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Wilbroad Mutafungwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kua mpaka sasa wanawashikilia watu watatu kwa mahojiano.

Aliwataja watu hao kuwa ni Neema Godfrey (41) mkazi wa Chamwino, Alphonce Boniface (19) na mtu mwingine ambaye jina lake halikutajwa kwa sababu za kiuchunguzi.

Naye mtendaji wa kata Chamwino, Bright Sospeter alisema, majira ya saa kumi jioni alisikia watu wakielezea tukio hilo wakiwa na hisia za kutokea mauaji, ndipo wakajumuika kama viongozi na kuenda eneo la tukio.

Alisema, walifanya upekuzi wa nyumba nzima na kumkuta baba huyo akiwa amefariki chooni huku pembeni yake kukiwa na mchi pamoja na damu sakafuni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *