Baba afikishwa mahakamani kwa kumbaka mwanae

 

 

Mkazi wa Mbezi Juu Said Rashid (36), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar es salaam kwa shtaka la kumbaka mtoto wake.

Mshtakiwa huyo alifikishwa katika mahakama hiyo Leo mbele ya hakimu Anifa Mwingira na kusomewa shtaka lake na Wakili wa serikali Matarasa Hamisi.

Wakili Hamisi alidai katika tarehe zisizojulikana kati ya Mwaka 2016 na Aprili 2019 eneo la Mbezi Juu, Wilaya ya Kinondoni mshtakiwa alimbaka mtoto wake (jina limehifadhiwa) ana umri wa miaka 13.

Mshtakiwa alikana kufanya kosa hilo na upande wa Jamuhuri ukieleza upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hakimu Mwingira alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria watakaotoa bondi ya Sh milioni moja kwa kila mdhamini.

Mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande mpaka kesi yake itakapokuja tena Juni 10 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *