Waziri Mahiga akiri serikali kusitisha mikataba ya wawekezaji

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Augustine Mahiga amesema serikali imekuwa ikisitisha mikataba ya wawezaji kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kutimiza masharti waliyokubaliana katika mkataba.
Dk. Mahiga aliyasema hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Ileje(CCM), Janeth Mbene .
Mbunge huyo alihoji ni mikataba mingapi imesitishwa na sekta ngapi zinaongoza? serikali imeingia gharama kiasi gani katika kesi zilizofunguliwa mahakamani kutokana na kusitishwa kwake.
“Je, serikali imepata faida au hasara gani kwa kusitisha mikataba hiyo,”alihoji.
Akijibu maswali hayo, Waziri Mahiga alikiri kuwa serikali imekuwa ikisitisha mikataba ya uwekezaji kutokana na sababu mbalimbali.
“Moja ikiwa ni upande mwingine wa mkataba kushindwa kutimiza masharti kwa mujibu wa mkataba au makubaliano ama inapobainika kulikuwa na udanganyifu ambao haukuwekwa wazi taarifa za msingi wakati wa kuingiwa kwa makubaliano au mkataba husika.
Alisema kwa sasa serikali bado inaendelea na mapitio ya mikataba yote iliyoingiwa ili kutambua kama vigezo na masharti katika mikataba hiyo vinatimizwa ipasavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *