WAKIMBIZI, WAHAMIAJI KUNUFAIKA

 

Shirika la afya duniani (WHO) limeazimia kuhakikisha wakimbizi na wahamiaji wanapata huduma bora za afya na zenye kiwango.

Hayo yamesemwa jana  katika mkutano wa bodi ya afya wa shirika hilo unaoendelea huko Geneva Switzerland ukijumuisha nchi wanachama.

Nchi hizo zimekubaliana mpango mkakati wa miaka mitano kuchukua hatua za kuhakikisha kundi hilo la watu wanapata huduma za afya ikiwemo upatikanaji wa dawa na chanjo.

Takwimu zinaonyesha, takriban watu milioni 10 wanaishi bila utaifa, makazi na kukosa huduma bora kama za afya, ajira na uhuru wa kujongeahuku idadi ya watu wanaolazimika kukimbia makazi yao ikifikia Milioni 68.5

Idadi ya wahamiaji imeripotiwa kuongezeka toka 173 mwaka 2000 na kufikia 250 mwaka 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 49%.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *