Nyalandu atafutiwa dhamana

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, anatafutiwa dhamana kwa sasa baada ya kukamatwa jana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Singida.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Vicent Mashinji amesema wanashughulikia dhamana ya Nyalandu.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida Joshua Msuya amethibitisha kuwa Nyalandu anahojiwa  kutokana na kufanya vitendo vinavyoashiria uwepo wa rushwa.

Nyalandu ambaye alishawahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii alihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chadema alikamatwa Jumatatu saa 9 alasiri mkoani Singida kwa ajil ya mahojiano na Takukuu.

Itaendelea…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *