Nyalandu apata dhamana

 

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amepatiwa dhamana pamoja na wenzake wawili kwa masharti ya kila mdhamini kuwa na amana ya Sh. milioni tano.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeeleza kuwa Nyalandu na wenzake wamepatiwa dhamana kutoka polisi mkoa wa Singida na wametakiwa kesho kuripoti asubuhi kituoni hapo.

Nyalandu alikamatwa jana na Taasisi ya Kuzuia na Kuambana na Rushwa (Takukuu) akiwa katika kikao cha ndani cha chama majira ya saa 9 alasiri na kwenda kuhojiwa.

Baada ya mahojiano hayo, Takukuru iliwarudisha katika kituo cha polisi cha mkoa  wa Singida kwa mahojiano na kupatiwa dhamana.

Awali, Mkuu wa Takukuru mkoani Singida Joshua Msuya alisema Nyalandu anahojiwa na Takukuru kutokana na kufanya vitendo vinvyoashiria uwepo wa rushwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *